MSANII anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina
Omary ‘Sabby Angel’ amedai ni mtaalamu zaidi pale linapokuja suala la
mahaba.
Sabby alisema kuwa anajiamini mno katika hilo kwani ni jukumu la mwanamke kumpa mapenzi mazito mtu yule anayempenda kwa dhati.
“Sio kwamba najisifu, lakini ukweli lazima katika mahaba uwe mjuzi
wa hayo mambo ili hata mumeo au mpenzi wako asitoke nje kabisa,”
alisema. Kuhusu kazi zake za filamu, alisema ataendelea kuhakikisha
anatesa zaidi ili kuwa juu siku zote.
Spoti Starehe