Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani umemfanya msanii wa Bongo
Fleva,Nuh Mziwanda kuondoka nyumbani kwa mpenzi ambaye ni msanii,Shilole
ili kumpisha mpenzi wake afunge kwani hawajafunga ndoa.
Shilole ameyazungumza hayo wakati akizungumza na Clouds Fm,ratiba
yake nzima ya mapishi kwenye mwezi Mtukufu na kusema kuwa mwezi huu wa
Ramadhani ameacha kufanya vitu vyote vya starehe na ndiyo maana hata
mpenzi wake Nuh ameondoka nyumbani kwake ili asiharibu funga yake.
‘’Nuh ameondoka nyumbani kwangu amerudi kwao ili asiharibu funga yangu,’’alisema Shilole.
Cloudsfm.com