Uzushi huo umekanushwa na kulaaniwa vikali na muigizaji mwenzake, Jacob Stephen aka JB.
“Ndugu zangu jana kupitia akaunti feki ya facebook kuna mtu alitoa picha yangu nikilia na kusema Irene Uwoya amefariki,” ameandika JB kwenye Instagram.
“Habari hii ya uongo ilileta shida kubwa katika familia yake na watu wa karibu. Leo tena asubuhi mwingine kasema nimepata ajali nakusababisha tafrani kubwa,” aliongeza.
“Napenda kuwaambia mashabiki wetu kuwa habari hizo ni za uongo. Tuko fiti kwa damu ya Yesu na tunavunja roho hizo za kunenea watu mabaya ktk jina la Yesu..amen.”
Bongo5