Wednesday, April 22, 2015

MAMA LULU ATAMANI MWANAYE AFE TU!

0
Imelda Mtema
Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!Lulu akiwa hoi nyumbani.
YOTE HAYA KISA MITANDAO
Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.
TUJIUNGE NA MAMA LULU
Akizungumza na gazeti hili, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.
MANENO KUNTU
“Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi.
“Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia.“Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?
“Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue,” alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Mzazi huyo aliendelea kusema kuwa, anaamini kwamba mambo mengine yanayotokea katika maisha ya mwanaye ni mipango ya Mwenyezi Mungu hivyo haoni sababu ya Lulu kubebeshwa lawama za ajabu.
Mama huyo alisema kuwa watu hao wanataka mwanaye afe kwa sababu kuna wakati anakosa raha ya dunia hivyo naye anatamani afe tu ili watu wamwache apumzike.
KIPINDI KIGUMU CHA MITIHANI
Mama Lulu aliendelea kueleza kuwa, Lulu kwa sasa yupo kwenye kipindi kigumu cha mitihani (anasoma Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Magogoni-Posta jijini Dar) lakini anawezaje kufanya vizuri huku kuna baadhi ya watu wakimsemea maneno yasiyofaa?!“Atawezaje kufanya vizuri wakati watu wanamwandama kila kukicha? Huko kote ni kumkatisha tamaa hivyo nimemwambia mwanangu amwachie Mungu na kusali sana,” alimalizia mama Lulu.Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’.
HUYU  HAPA LULU
Baada ya kuzungumza na mama huyo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu ili kumsikia na yeye ana mtazamo gani kuhusu shutuma hizo ambapo alisema kila kitu anamuachia Mungu pekee na si mwingine hivyo kwa sasa aachwe asome.“Kila kitu changu nimemuachia Mungu maana hakuna mtetezi wangu zaidi yake, ndiyo maana ninasali sana ili Mungu anisaidie,” alisema Lulu.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment