Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.