Saturday, February 28, 2015

UBUYU:Baada ya Kupata Pedeshee Mpya, Wolper Kubadili Dini tena

0
UBUYU:Baada ya Kupata Pedeshee Mpya, Wolper Kubadili Dini Tena!!Mrembeo na mwigizaji wa filamu, Jackline Massawe Wolper, kwa mara nyingine ameripotiwa na gazeti moja la udaku kuwa kuangukia kwenye mikono ya pedeshee ambaye ndiye anayempa jeuri ya fedha kwa sasa.

Pedeshee huyo anayedaiwa kumpangishia nyumba ya kisasa mrembo huyo na kumpa jeuri ya kufanya matanuzi hapa mjini, anadaiwa kutaka kumbadili dini staa huyo ili awe muislam kwa mara ya pili.

Licha ya maisha yake kubadilika na kuwa na mkwanja mrefu, Wolper mwenyewe amekuwa akifanya siri juu ya maisha yake mapya yenye neema kutoka kwa mwanaume huyo ambaye ndiye ATM yake kwa sasa. kwa kuhofia kupatwa na aibu kama sio fedheha kama ilivyotokea kwa aliyekuwa laaziz wake maarufu kwa jina la Dallas, mrembo huyo ameamua kufanya siri kubwa juu ya mahusiano yake mapya kwa kuogopa wambea wa mujini.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment