Exclusive, H Baba msanii anayewakilisha Mwanza Rock City amemwambia MrInfo kuwa wiki moja nyuma gari yake ilivunjwa kio na baadha ya thamani kuibiwa na wezi.Tukio hilo limetokea mitaa ya Lumumba Kariakoo jijini Dar es salaam na kwamba mmoja ya vitu muhimu vilivyoibiwa ni chombo cha kutunzia nyimbo na mambo yake tofauti yani flash disk.
H Baba anasema kwenye Flash Disk palikuwa na wimbo Tubebane ambayo ndio imevuja ila pia kulikuwa na nyimbo mbili,Moja aliyofanya na Fally Ipupa na nyingine na msanii kutoka hapa Tanzania.
H Baba ameonyesha kutofurahishwa na uvujishaji wa nyimbo hio na kusema mwizi huyo ataharibu mipango yake kama atavujisha nyimbo yake na Fally Ipupa.