Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia hatua nyingine ambapo sasa washiriki wa fainali ya Shindano hilo kuanza kupigiwa kura na watazamaji. Washiriki hao 20 kutoka kanda sita za Tanzania wanaendelea na kambi huku wakipewa mafunzo juu ya sanaa ya uigizaji na uandikaji wa muswada (script) kutoka Kwa Mhadhiri wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Dk Mona Mwakalinga.

Washiriki hao 20 sasa watapigiwa kura na watazamaji kutoka na
kuonyesha uwezo wao wa kuigiza na kuwavutia watazamaji kwa vipaji vyao.
Kipindi cha Kwanza cha Mchujo kimeonyeshwa hapo jana Kupitia kituo cha
Runinga cha ITV ambapo sasa watazamaji wameweza kujionea uwezo wa kila
Mshiriki katika Shindano hilo.
Vipindi vya TMT vitaendelea kurushwa kupitia ITV kila Jumamosi saa NNE USIKU na kurudiwa Jumapili Saa KUMI JIONI na JUMATANO SAA TANO USIKU, usikose kutazama ni mshiriki yupi mwenye uwezo na aliyekuvutia ili uweze kumpigia kumpigia kura.
Jinsi ya Kumpigia Kura Mshiriki umpendae unaenda upande wa Meseji kwenye Simu yako na Kuandika "TMT" ikifuatiwa na Namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda 15678. Mfano: TMT00 halafu unatuma kwenda 15678. Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents litafanyika Mwisho wa
Mwezi wa Nane ambapo mshindi mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi
Milioni 50 za Kitanzania.