Maisha ya kimuziki ya wasanii wengi wa Tanzania walio wahi kufanya
show nyingi kipindi cha nyuma wanaweza kuwa mashuhuda wa hiki
alichokizungumza Madee kupitia Exclusive interview na millardayo.com.
Asilimia kubwa ya wasanii wa bongo fleva kipindi cha nyuma hawakua
wakilipwa malipo kama haya ya sasa,miongoni mwa wasanii hao ni Madee
ambaye amesema>>Dah kiukweli hela ndogo niliyowahi kulipwa
nakumbuka ni 40,000′
‘Hahaha ilikua mwaka 2003/2004 wakati nimetoa wimbo wa kazi yake mola
alituita promota mmoja ambaye hivi sasa hivi ni marehemu anaitwa
Mnomba,nakumbuka nilienda mimi na babu Tale baadae tukakutana na
Dudubaya huko’
‘Tulikuwa tuna enjoy maana hakuna mtu aliyekua anajua kama haya ni
maisha show hiyo ilifanyika Triple A,malipo makubwa niliyowahi kulipwa
ni mwaka jana 2013 kwenye show za vinywaji baridi nililipwa Milioni 38
kwa show 5′
‘Mkataba aliusaini Babu Tale nikashangaa Babu Tale amekuja akaja
katoa hela akasema hela hizi hapa tugawane ni za show zako 5 ilikuwa
mwezi wa kwanza nakumbuka’.
Madee kwa sasa kaachia wimbo wake mpya unaitwa Ni sheeda ambao umefanyika kwa Marco Chali.
