Vikwazo vya Marekani kwa Uganda kama adhabu, vinajumisha kuwapiga marufuku wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kutoingia Marekani.
Marekani itapunguza ushirikiano na Wizara ya Polisi na Afya za Uganda, na kuachana na mpango wa mazoezi ya kijeshi kati ya wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa Uganda.
Uganda walipitisha sheria ambayo inaeleza wazi mtu atakayekutwa na hatia ya kushiriki katika masuala ya ushoga atahukumiwa kifungo cha maisha jela.