Saturday, June 14, 2014

Idadi Ya Maombi Ya Kumshirikisha Mwana FA Baada Ya Kutoa Mfalme

0
 Mwana FA ni bondia wa hip hop mwenye mistari konde mizito kila anapoachia wimbo, lakini gospel hip hop ya Mfalme aliyomshirikisha G-Nako imeongeza kitu kikubwa zaidi kwenye muziki wake.
Rapper huyo ameeleza kuwa baada ya kuachia wimbo wa Mfalme, amepata maombi ya wasanii zaidi ya 13 ndani ya mwezi mmoja wanaotaka kumshirikisha kwenye kazi zao.
Kwa mujibu wa Mwana FA, itambidi achague collabo chache kati ya hizo kwa kuwa sio rahisi kuzifanya zote ndani ya mwezi mmoja. Amesema kama atafanya collabo zote hizo ndani ya kipindi hicho kifupi sauti yake inaweza kuchosha kwa kuwa anaweza kuwa anasikika muda mwingi radioni.
Kwa upande mwingine, Mwana FA amepanga kufanya video ya wimbo wake ‘Mfalme’ wiki ijayo na atafanya na muongozaji Kevin Bosco Jr aliyefanya video ya wimbo wa AY, Asante
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment