Saturday, June 14, 2014

Hii Ni Kuhusu Video Ya Wimbo Mpya Wa Diamond Aliofanya Na Iyanya Nchini Uingereza

0
Mwezi uliopita tulisikia Diamond amefanya ngoma na wasanii wengi wakubwa wa Nigeria akiwemo mkali wa Kukere, Iyanya.

Diamond na Iyanya walishuti video ya wimbo huo nchini Uingereza na tayari Afrika imeanza kuiona kupitia kituo cha runinga cha Channel O japo television za Tanzania bado hazijaupata.
Akiongea katika kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio, Diamond ameeleza kuwa aliwatumia video hiyo mapema lakini hakuwaambia kuanza kuicheza. Lakini amewahakikishia mashabiki wake kuwa video hiyo itaanza kuonekana rasmi kwenye vituo vingine vya kimataifa kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.
Platinumz ambaye ameachia wimbo mwingine mpya wiki unaoitwa Mdogo Mdogo ameeleza sababu za kuachia nyimbo mbili kwa wakati mmoja.
“Nimeplan kuachia wimbo wa kimataifa na wa asili ya nyumbani na sababu ya kufanya hivyo, unajua watanzania tulivyo ukitengeneza nyimbo ya international yenye asilimia 50 ya vizungu usifikiri kila mtu ataipenda. So na mimi market target yangu ilikuwa sehemu nyingine kwa sababu nafanya hii kazi nyumbani lakini nataka soko la nje.”
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment