Mwigizaji wa maarufu wa filamu wa nchini Marekani Angela Basset
anatarajia kuongoza filamu itayohusu maisha halisi ya aliyekuwa
mwanamuziki nguli duniani Witney Houston.
Kituo cha Televisheni cha Lifetime cha Marekani kimethibitisha kuwa
filamu hiyo itaelezea maisha ya Witney hadi kuibukia kwenye umaarufu
pamoja na mahusiano yake na aliyekuwa mume wake kwa kipindi hicho Bobby
Brown kuanzia mara ya kwanza walipokuna hadi kufunga ndoa.
Mwanamuziki Witney Houston alifariki dunia February mwaka 2012 akiwa
na umri wa miaka 48. Witney alikuta amekufa chumbani kwake katika hoteli
jijini Los Angeles.
Angela Basset amecheza filamu nyingi zinazohusu maisha halisi ya watu
ambapo pia aliwahi kucheza filamu ya hayati Notorious BIG akiwa kama
mama yake na kutumia jina la Voletta Wallace.