Weusi ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanaojua kutumia jina na kazi zao kujiingizia kipato zaidi nje ya muziki. Awali kwenye video ya Gere tuliona nguo na mavazi tofauti ikiwa ni awamu ya kwanza ya ubunifu wa vijana hawa na jinsi wanataka kuteka wateja wao. Jipya kutoka weusi sammisago.com napenda kukufahamisha kuwa vijana hawa wametambulisha miwani za weusi zenye Neno GERE, yani upande wa kushoto ni GE Nakulia ni RE Kwenye miwani hizo.
Miwani hizi zitaingia sokoni Kuanzia May 29 2014. Joh Makini anasema ni ubunifu wa rafiki anayeishi na kufanya kazi zake Arusha, aliwakilisha ubunifu na wazo lake likakubalika na wanafanya nae kazi. Bei ya miwani itatajwa siku yeyote sasa.
Miwani hizi zimeongezeka kwenye orodha ya bidha za weusi vikiwemo Top za kike, Kofia, Tracksuit na T Shirt.