Hatimaye Rapa maarufu wa muziki wa nchini Marekani Kanye West na
mwanadada anayemake headlines kila kukicha Kim Kardashian wamefunga
pingu za maisha na kuwa mume na mke huko Florence nchini Italia. Wapenzi
hao walisafiri kwa nyakati tofauti kutoka jijini Paris nchini Ufaransa
ambako waliungana na familia zao katika ile Pre Wedding Party.
Taarifa zinadai kuwa wanandoa hao wapya walipanga kufunga ndoa hiyo
huko Chateau de Versailles lakini sheria za Ufaransa hazikuwaruhusu
kufanya hivyo kutokana na hata mmoja wao kutokuwa na uraia wa nchi hiyo.
Cha kushangaza ni kwamba si Jay Z wala Mke wake Beyonce aliyehudhuria
katika harusi hiyo na kuishia kutuma salamu za pongezi licha ya kuwepo
kwa uvumi kuwa Jay Z atakuwa msimamizi wake kutokana na ukaribu na
urafiki mkubwa waliokuwa nao.
Tukio hilo kubwa limehudhuriwa na wageni mbalimbali na watu mashuhuri
akiwemo mwanamuziki John Legend na mkewe Chrissy Teigen na muongozaji
wa filamu ya 12 Years a Slave Steve McQueen.
Story nyingine kubwa ni kwamba mabosi wa kampuni ya Adidas pia
walichagua siku hiyo ya harusi kuzindua tangazo lao la kombe la dunia
kwa mwaka 2014 linalomhusisha rapa Kanye West pamoja na mastaa wakubwa
wa soka duniani Lionel Messi na Dani Alves.