MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo
Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema anashindwa
kumtathimini msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha kutokana na
kujitenga na wasanii wenzake.Msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha.
Akifafanua kauli yake, Steve alisema mwanadada huyo anamshangaza
sababu hajui yupo kundi lipi kwa kuwa kwenye Bongo Movie hayupo na wala
hana kadi ya chama chochote akiwa kama msanii na mbaya zaidi hajitokezi
kujumuika na wenzake.“Hana
kadi ya chama chochote na isitoshe anajitenga na wasanii wenzie,
hahudhurii kwenye shughuli yoyote ile iwe ya huzuni au furaha, kiukweli
simuelewi, abadilike,” alisema Steve.
Paparazi wetu alipomtafuta Baby Madaha kuzungumzia ishu hiyo alisema
ana mambo mengi ya kufanya ndiyo maana huwa hashirikiani na wenzake,
akipata nafasi atahudhuria.