Kama upo Dar es salaam na huwa unapita barabara ya zamani ya kwenda
Bagamoyo najua hili eneo karibu na Shoppers Mikocheni mvua zinaponyesha
lazima huwa linakupa kero kwa sababu mvua kidogo tu huwa inahamishia
bahari.
millardayo.com imekutana na
mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambae hili ni eneo lake na anasema
‘Manispaa yetu ya Kinondoni kuanzia mwaka 1995, 2000 na 2005 watu
walifanya kama ni shamba la bibi, kila mtu alikua anachuma anachotaka
pasipo kujali mipango miji ikoje ama sheria zinasema nini’
‘Matokeo yake ni kwamba yale maeneo ya Shoppers na Tanesco yote
yalikua ni maeneo ya mkondo wa maji na kuelekea kule kwa Warioba yalikua
ni maeneo ya wazi ambayo maji yalipokua yakitoka huko ukanda mwingine
yanapita hapo kuelekea baharini’
‘Sasa Wachakachuzi wa viwanja enzi hizo wakauza haya maeneo na watu
wakajenga majengo yao yakaziba mifereji ambayo ilikua imetengenezwa kwa
makusudi ya kupeleka maji baharini sasa mvua zikinyesha maji yanajaa,
sasa maskini kuna Wananchi wangu wa bonde la mpunga kule yani ndio
wanaathirika zaidi pamoja na wapita njia hivyo ikabidi tutafute pesa
kupitia mfuko wa barabara na sasa kazi inaendelea’‘Hii ni project ya kujenga mifereji ya kisasa kwenye eneo hili na
itagharimu shilingi BILIONI SITA, sasa u can imagine kama kusingekua na
uzembe uliofanyika huko nyuma kwa watu ambao walipewa dhamana ya
Kinondoni hii BILIONI SITA ingewezekana ikajenga vibarabara vingi sana
vya ndani jimbo la Kawe’
‘Bilioni sita hii itatumika kujenga mifereji mikubwa ambayo itaanzia
pale Mikocheni A darajani mpaka huku TANESCO alafu itashuka kuelekea
baharini na itasaidia sana Wananchi wangu wa bonde la Mpunga ambao
wanateseka sana, inajengwa lami kwa mara ya kwanza barabara ya Maandazi
(Maandazi road)’‘Hii mvua ikiisha na zile project zikiendelea vizuri hiyo miaka ya mbele
inayokuja itakwenda vizuri lakini zaidi wote ambao wanatumia barabara
ya Bagamoyo ya zamani kwenda Mikocheni, Mabwepande, Kawe na wengine
wanaopata mafuriko, kwa ukubwa wa makaravati niliouona naamini
itapunguza kero hii kwa muda mrefu, project ya mifereji haitakiwi
kuchukua miezi sita ila hii mvua imevuruga mambo mengi sana’