Tuesday, April 8, 2014

JE WAJUA HALIMA KIMWANA AFUNGUKA KUHUSU MASTAA KUMTONGOZA DIAMOND

0

Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo

Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.

Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.

Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.

CREDIT - GPL
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment