Miezi
ikapita, mawiki yakasonga hatimae siku, masaa na dakika zake zikapotea
na sasa EFM inayopatikana katika masafa ya 93.7 imesikika hewani kwa
majaribio kwa mara ya kwanza.
Redio
hii iliobeba watangazaji mahiri, waandaaji wa vipindi wenye umakini, ma
DJ wanao sadikiwa kuwa walishushwa kwa ajili ya kazi hii, uongozi
thabiti na yenye usikivu mujarab, habari zake zilianza kupenya kwenye
masikio ya washashi mwishoni mwa mwaka jana na kupelekea wamiliki na
wadau wa redio nyengine kukosa usingizi na hata siku wakiupata basi
huweweseka usiku na kupiga mayowe ama kujikuta wakikosa hata nguvu ya
kuzuia haja ndogo kutoka.
Redio
hii itadili kwa asilimia 85 na burudani...na watakaoongoza balaa hilo
ni watu wenye kulijuwa game kwa kipindi kirefu saana na burudani
iliolengwa hapa hakika ndio mwiba mchungu utaowatesa weengi
waliowanyonya na kuwanyanyasa wasanii kwa miongo kadhaa sasa.
Kuna Minong'ono kuwa inamilikiwa na Lady Jay Dee....Kwa mwenye Ukweli Funguka Hapa basiiiii....
Nanga
ndio imeshainuka, Unyonyaji ndio umekwisha, Wanyonge mtafarijika, Game
sasa litabadilika, Walio Vilaza wataaibika, makini watasikika, Sina
imani nina hakika.