“Imefikia point ambayo inaweza kufanya kile kitu ambacho naweza kufanya lazima nitafute production ambayo iko fresh, kwa sababu nimechunguza video nyingi za kitanzania zinashindwa kupata airtime kwa sababu audio zake zinakuwa miyeyusho, labda director anajitaidi kwenye video amefanya poa ila kwa sababu audio yake inazingua basi hiyo video haiwezi kupata airtime kwenye tv station mbalimbali”.
Pia Linex aliongeza kuwa kilichompeleka kwa Marco Chali ni kwamba kupitia ngoma yake hiyo ambayo inaitwa ‘Yuenai’ ambayo amesisitiza zaidi kwa suala zima la kuwekeza katika mziki wake.
“Hauwezi ukafaulu kama huwezi ‘Kuwekeza’ kwenye kitu ambacho unakitaka, kama unafanya biashara lazima uwekeze ili uweze kupata ulichokipanda na ndiyo maana hata mimi nafanya biashara ya mziki kwa iyo nainvest ili nipate chapaa”. Aliongeza Linex