Mansu-Li ambaye hufananishwa sana na rapa Nas Escobar kutokana na mistari na muonekano wake ameongea na eNewz kuwa hivi sasa anasoma katika chuo cha uhasibu cha T.I.A Mtwara Campus na kusema kwamba atakuwa akiachia ngoma kama kawaida ila kuonekana jukwaani itakuwa ngumu kwa sasa.
Hivi sasa Mansu-Li tayari ana kazi yake mpya ambacho inatarajia kutoka hivi karibuni iliyobatizwa jina ‘Kila Sababu’ traki ambayo imepikwa ndani ya Tongwe Records akimshirikisha msanii Damian Soul.
Aidha, rapa huyo anayefanya vyema na albamu yake ilioyobatizwa Kina Kirefu ameongeza kuwa baada ya kufanya kazi na Jaymoe, Belle 9 na Niki Mbishi hivi sasa mashabiki wakae tayari kwa ajili ya traki hiyo mpya ambayo itasambazwa na CEO wa Tongwe Records aitwaye Jumior aka Murder.