Ni aibu jamani, kama bado hamjafikia level hiyo ya lugha, acheni tu, wekezeni zaidi kwenye kiswahili basi ieleweke tu kwamba movie ni ya kiswahili. Au kama mnataka mpate soko la kimataifa, hebu mu-invest sana mpate professionals wanaoweza kuwaandikia lugha ya kueleweka, otherwise mnajiabisha na kuiabisha nchi hii, can you imagine unaeangalia movie ndo unaona aibu kwa niaba yao. Maana ile lugha inayoandikwa pale si english, bali direct translation from kiswahili inaishia kuwa pigini, au mnajaribu kutengeneza lugha ingine? Mi sijaelewa jamani.
Kama vipi muwe mnaniletea japo nina uelewa mdogo wa hii lugha naamini i can do better than that. Ni ushauri tu, najua kina Kanumba sijui Ray huwa mnapita humu, next time kwenye baraza lenu la wasanii hebu wekeni hii kama agenda, naamini wapo watu kibao ambao hata kwa kuvolunteer wanaweza ku edit na kusaidia kutoa lugha inayoeleweka.