Dr Cheni ameiambia Bongo5 kuwa mpaka sasa hajui ni maajabu gani yametokea mpaka filamu hiyo kupendwa kiasi hicho.
“Kwa kawaida ndani ya wiki moja huwaga tunauza nakala elfu 5,000. Lakini kwenye filamu ‘Nimekubali Kuolewa’ imenifungulia njia,” amesema.
“Toka naanza kufanya filamu sijawahi kuuza filamu elfu 20,000 ndani ya wiki moja. Ni dalili nzuri kwangu na inanifanya nione kumbe nilichokifanya ni kitu kikubwa sana. Namshukuru Mungu, waandishi wa habari pamoja na mashabiki wangu,” amesema Cheni.
Bongo5