Sunday, May 3, 2015

Chadema yakutana Dar kujadili kuongoza Seriklali ya Awamu ya Tano

0
Dar es Salaam. Chadema, ambayo imekuwa ikieleza matumaini yao ya vyama vya upinzani kutwaa dola mwaka huu, leo inaanza kikao cha Kamati Kuu, huku moja ya ajenda ikiwa ni kuzungumzia kuongoza Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Chadema inaeleza kuwa moja ya ajenda hizo itakuwa ni “kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza Serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu”.
Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa, Uchaguzi Mkuu, kupokea na kujadili taarifa ya mwenendo ya majadiliano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), yanayohusisha vyama vinne vya upinzani ambavyo vimeazimia kusimamisha mgombea mmoja wa udiwani, ubunge na urais.
Katiba ya Wananchi (Ukawa), yanayohusisha vyama vinne vya upinzani ambavyo vimeazimia kusimamisha mgombea mmoja wa udiwani, ubunge na urais.
tayari Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi vimeshakubaliana kwa asilimia 95 kuhusu kusimamisha mgombea mmoja na bado havijaafikiana katika majimbo 12.
Ingawa vyama hivyo vimekuwa vikaituhumu Serikali kutengeneza mazingira ya kuibeba CCM kwenye uchaguzi ujao, Chadema imeshaeleza wazi kuwa itashinda wapinzani watashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na kwa mara ya kwanza nchi itaongozwa na wapinzani, kwa mujibu wa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.
Pia kikao hicho kitajadili, taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama.
Agenda nyingine zitakazojadiliwa ni taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanzania Bara na Zanzibar na mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapigakura katika Daftari la Kudumu kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).
Chadema imekuwa ikiituhumu Serikali kuwa inaendesha kazi hiyon ya kuandikisha wapiga kura kwa kusuasua na kueleza hofu yake kuwa hizo ni njama za kutaka Serikali ya Awamu ya Nne iongezewe muda.
Inadai kuwa vifaa vilivyowasili hadi sasa ni vichache hivyo kuna uwezekano suala hilo likasababisha Uchaguzi Mkuu kusogezwa mbele.
Mbali na hayo, kuna uwezekano mkubwa pia wakajadili suala la kupata mgombea urais na makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano atakayepeperusha bendera ya Chadema katika mchujo wa kumpata mgombea mmoja wa Ukawa, suala ambalo katika kikao cha umoja huo lilibaki kama kiporo.
Dk Slaa alisema kuwa suala hilo kwa upande wa Zanzibar limekamilika bado upande wa Bara.Licha ya kuelezwa kuwa wameshafanya ugawaji Majimbo yote, suala jingine ambalo Chadema wanaweza kulijadili katika kipengele cha hali ya kisiasa ni msuguano wa ugawanaji majimbo, ikiwamo baadhi ya vyama kupewa majimbo machache tofauti na waliyoomba kama vile NLD iliyoomba 35 na kupangiwa mawili pekee.
Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alisema licha ya kupewa Majimbo machache iwapo atayakosa hawezi kujiondoa Ukawa.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment