SAFARI ya mwisho ya mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection na Meneja wa kundi hilo, Abdul Bonge, leo ilianzia nyumbani kwake Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam mwili wake iliposafirishwa kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi.
Wakati mwili wake ulipowasili nyumbani kwake kutoka Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi, umati wa waombolezaji uliangua kilio na kusababisha hali ya kutosikilizana.
(PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)