Staa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ amefunguka kwa kusema kuwa sinema zake si kuangalia filamu gani imeingia sokoni na kufanya vizuri kwa staili fulani na yeye akakurupuka na kutengeneza filamu kwa mlipuko.
“Mara nyingi wapenzi wa sanaa si rahisi wanapenda nini? Lakini ninawajua wapenzi wa filamu zangu hivyo inakuwa vigumu sana kujiingiza katika filamu za mlipuko, baada ya filamu moja kufanya vizuri, basi kila mtu anatoka na staili hiyo hiyo,”anasema Ray.
“Tumeshuhudia filamu kama Chausiku, na nyinginezo zilizotengenezwa katika maandhari ya maisha yetu mitaani basi kila sinema ni hivyo hivyo, ni wazi inaonyesha kuwa hatuamini mawazo yetu,”anasema Ray.
Ray anasema kuwa ukitengeneza filamu ya msimu pia msimu ukiisha watu wanaisahau na kuendelea sinema nyingine lakini pia wapenzi wa filamu Bongo Movies hawataki filamu kubwa zilizotengenezwa kwa akili nyingi, akatolea mfano wa sinema ya Crazy ya marehemu Kanumba haikufanya vizuri.