Mwanamuziki ambaye pia ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameshangazwa na madai kuwa eti mimba ya mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ imetoka na kuwataka Wabongo kuacha tabia ya uzushi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake zari.
Akizungumzia madai yaliyokuwa yamezagaa mtandaoni kuwa ile mimba yake aliyokuwa akiilea kama yai kwa Zari imechoropoka, Diamond alisema:
“Hee! Eti mimba ya Zari imetoka! Wanaosema hivyo walaaniwe. Mbona Wabongo wazushi sana, itakuwaje hivyo halafu nisijue. Zari yuko fiti