Saturday, February 28, 2015

Kapteni Komba afariki, aacha mjane na watoto 11

0
Waombolezaji wakimfariji mke wa marehemu Kepteni John Komba nyumbani kwake maeneo ya Tangi Bovu jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Herman 


Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .
"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment