Saturday, July 12, 2014

JE WAJUA JINI KABULA ACHARUKA VIMINI MWEZI RAMADHANI

0
STAA wa sinema za Kibongo, Miriam Mjolwa ‘Jini Kabula’ amecharuka baada ya kukosolewa juu ya mavazi ya mitego, vimini, anayovaa ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Baada ya majirani wanaofunga kufikisha malalamiko, paparazi wetu alimvutia waya Jini Kabula na kumsomea mashtaka hayo ambapo alisema kuwa alikuwa lokesheni siku waliyomuona lakini pia hahofii sana kwani mwezi huo haumuhusu.

“Hao wanaweka chumvi tu mimi sikuwepo huko mtaani nilikuwa lokesheni tangu mwezi uanze, na hata kama nitavaa nguo za ajabu, mwezi huu haunihusu nitavaa vyovyote nipendavyo,” alisema Jini Kabula.



 
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment