Sammisago.com ilipiga story na Nuh Mziwanda ili kuyakusanya majibu yote na kufahamu kiundani kuhusu uamuzi wake.
Mziwanda alieleza kuwa tattoo aliyochora ni ya kudumu katika kipindi chote atakachokuwa duniani na kwamba haitafutika mpaka siku anaingia kaburini.
“Nilimwambia labda wewe ndio utakaekuja kunizingua lakini mimi hata siku moja sitakuzingua. Hata kama tukiachana, mimi nimeamua hivyo na nimefanya kwa mapenzi yangu kwa sababu nampenda sana na ni mtu muhimu sana kwangu.”
Kwa upande wa Shilole, alipost picha hiyo kwenye Instagram na kuandika ujumbe wa kumshukurua mpenzi wake. “Thanx my lv 4 dis! Umeonesha lv ya ukweli”