Zitto alivutiwa na ujumbe wa wimbo huo unaohusu watu kutolipiza kisasi na kuendelea kumtegemea Mungu katika kila jambo. Baada ya kuguswa alimfuata Adam Juma na kulipia video hata bila kumwambia Linex, baadae akampa taarifa ajiandae kushuti.
“Tunaanza kushuti next week kwa sababu nilikuwa bado niko busy na Kili Tour. Ni wimbo mzuri utakaoigusa sana jamii halafu baadae tukishashuti tutajua mambo mengine.”