Friday, June 20, 2014

Msami Athibitisha Uhusiano Wake Na Uwoya, Mipango Na Tofauti Ya Umri Wao

0
Mwimbaji na mwalimu wa kucheza Msami amefunguka kuhusu uhusiano wake na muigizaji Irene Uwoya baada ya mengi kuandikwa.Msami na Uwoya“Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.”
Akiongelea umri ulipo kati yao ambao wengi wanadai kuwa amezidiwa sana umri na Uwoya kwa hi ni kama Serengeti boy wake, Msami amesema yeye ni mkubwa zaidi ya Uwoya.
“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Amesema Msami.
Kuhusu mipango yao, amesema wako vizuri na wanafanya filamu yao itakayokuwa inahusu muziki na dance na Msami ndiye mhusika mkuu. Ameeleza kuwa bado hawajapanga jina la filamu hiyo na tarehe ya kutoka lakini itaingia sokoni mwaka huu.
Credit: Timesfm.co.tz
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment