Kocha mbrazil aliyewahi kuifundisha Taifa Stars kwa msaada wa rais wa
Jakaya Kikwete, Marcio Maximo ataingia Jangwani kuinoa timu ya Yanga.Kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti Maximo aingia Dar es Salaam siku nne baada ya leo (Jumamosi).
Hivi sasa Maximo yuko Brazil akifanya kazi ya uchambuzi wa kombe la dunia katika television ya taifa ya Mexico na anamaliza mkataba wake Jumatatu.
Klabu ya Yanga imethibitisha safari ya Maximo kuja Tanzania na kwamba ameanza maandalizi tangu juzi.
Wakati Yanga wanamleta Maximo kukinoa kikosi chao, bado wapinzani wao wa jadi Simba wako kwenye mchakato wa uchaguzi ulipangwa kufanyika June 29.
