Jana mida ya saa sita kasoro usiku maeneo ya Kimara mwisho, Msanii wa
Bongo Fleva Walter Chilambo akiwa na gari yake aina ya Passo rangi ya
Brown aligongwa mbele na gari lingine na aliyesababisha ajali hio
kukimbia. Walter hajapata madhara yeyote na mida hii yupo kwenye
mitikasi ya kurekebisha gari yake. Pole kwa Walter kwa kuingia gharama
ya kurekebisha gari yako.
Walter anasema “Waliomgonga usiku wa
15/May/2014 ni vijana zaidi ya watano waliokuwa kwenye gari aina ya
Noah. Walikuwa kwenye mwendo wa kasi sana kama wametoka kuiba au kufanya
tukio mahali flani. Walinipigia honi sana na makelele niwapishe huku
nikijaribu kuwapisha waligonga gari yangu makusumbe kwa mbele na
kuendelea kulisukuma pembeni mwa barabara”
Walter anaendelea kusimulia kuwa ” baada ya
vijana hao kukimbia alibaki na hofu na mshtuko mkubwa sana na kubaki
barbarani kwa muda mrefu akisubiri kutulia ndio aendele na safari”