Muziki wa dansi Tanzania Mei 15 ulipata msiba ambao umekua ni pigo
kwao na Tanzania kwa ujumla,ni msiba wa Amina Ngaluma ‘Japanese’ ambae
amefanya kazi kwenye bendi tofauti tofauti hapa Tanzania ikiwemo African
Revolution ‘Tam Tam’ pamoja na Double M Sound.
Taratibu za mazishi kwa mujibu wa mume wa Marehemu Amina Ngaluma Mr
Rashid Sumuni amesema wanasubiri mwili wa marehemu ufike na unategemewa
kuingia wiki ijayo kutoka Thailand alipokua akifanyia kazi.
Taratibu za mazishi Sumuni amesema kuwa mwili utazikwa maeneo ya huko huko Kitunda Machimbo,millardayo.com imefika hadi nyumbani kwa marehemu ulipo msiba huu ,hizi ni baadhi ya picha za nyumbani kwa marehemu.Baba mzazi wa Marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’Mume wa Amina Ngaluma Mr.Rashid Sumuni