Hata hivyo,
ikiwa msanii huyo ambaye kwa fikra zake anaamini ndiye mkali kuliko
wachekeshaji wote Bongo japokuwa Mzee Majuto ndiye namba moja, anaweza
kuwa mwerevu badala ya kuendelea kuwa mjinga.
KWA NINI MJINGA?
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford – Toleo la Pili) inamuelezea mjinga kuwa ni mtu asiyejua kitu au jambo fulani.
Hata hivyo, mjinga hawezi kuendelea kubaki katika hali hiyo baada ya kufundishwa na kujua maana.

HABARI KAMILI
Tukio la Mpoki hivi karibuni kuwadhalilisha watu waliofika jukwaani kukabidhi tuzo kwa washindi katika Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ni ushahidi tosha kuwa ana tatizo la kufikiri.

Ukiachana na
tukio hilo, rekodi yake ya maisha yake ya kisanii na nje ya sanaa
inathibitisha asivyo hodari wa kutumia ubongo wake sawasawa, vijana wa
mtaani huita zero brain (0).
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi anavyoigiza huwa anawasema watu vibaya hata wale ambao wamemsadia kufika alipo kisanii.
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi anavyoigiza huwa anawasema watu vibaya hata wale ambao wamemsadia kufika alipo kisanii.
TUZO ZA KILI
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye mjinga na anayejitambua, Mpoki asingeweza kumkejeli mtu mwenye heshima zake kama Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa Aset.
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye mjinga na anayejitambua, Mpoki asingeweza kumkejeli mtu mwenye heshima zake kama Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa Aset.
Asha anaweza
kuwa mama yake lakini bila haya alimwambia mbele ya hadhara kuwa kwa
alivyo na mwonekano mzuri kwa usiku ule, asubuhi yake angeweza
kusalimiwa shikamoo (akimaanisha angekuwa na mwonekano wa kizee kwa kuwa
hatakuwa na make up tena).
Hakuishia
hapo, Mpoki alifikia hatua ya kuingilia hadi mambo binafsi ya watu
ambayo katika hali ya kawaida hayawezi kuwa utani, alimwambia Maimartha
Jesse kuwa licha ya kwamba ananyonyesha lakini amepiga matiti jeki.
Upuuzi mtupu!
NJE YA KILI
Ukiachana na kero alizotoa kwenye jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana tabia ya kuwadhalilisha watu hata anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo mingi.
Ukiachana na kero alizotoa kwenye jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana tabia ya kuwadhalilisha watu hata anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo mingi.
Kutokana na
kile kinachoonekana kutojielewa, Mpoki humkejeli mtu makusudi ili
kutengeneza bifu akiamini magazeti yakimwandika ataendelea kuwa juu.
Hivi
karibuni alitoa wimbo ambao ndani yake amewatukana baadhi ya watu
akiwemo mwandishi mmoja mashuhuri nchini wa magazeti pendwa kwa kumuita
dada wakati akijua ni mwanaume (anapenda misala).
Kwa akili
zake fupi, aliamini paparazi huyo angepaniki na kurushiana naye maneno
kwenye magazeti na mitandao ya kijamii, hakufanya hivyo na mpaka sasa
yuko kimya kabisa kama hakuna kitu kilichotokea kwa sababu ni mwerevu.
Pia jamaa
huyo bila haya wala soni aliwahi kuigiza kwa kumkejeli Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwenye maigizo yao ya Orijino Komedi.
Ikumbukwe
kuwa, Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) inayomilikiwa na mzee Mengi
ndiyo iliyorusha kipindi chao cha vichekesho kwa mara ya kwanza. Kifupi
ndiye aliyemtoa baada ya kupigika kwa muda mrefu.
Mpoki
alitambulishwa kwa mara ya kwanza na Runinga ya ITV akiwa na Kundi la
Nyota Ensemble kupigtia Kipindi cha Mambo Hayo cha ITV ambacho ni mali
ya mzee Mengi.
WADAU WACHARUKA
Wadau wa burudani Bongo waliopata kuzungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, walionesha hisia zao za wazi kwa namna walivyokasirishwa na msanii huyo mwenye mdomo mchafu na asiyepima maneno.
Wapo waliokwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba ikiwa kutakuwa na shughuli yoyote ya kiburudani na msanii huyo akapangwa kuwa MC basi hawatahudhuria kwa kuogopa kudhalilishwa.

Nasra
Abdillah wa Tabata jijini Dar alisema: “Mimi nahisi kuna kitu cha zaidi
kwa Mpoki, si kwamba ni mchekeshaji, nadhani kichwani hayupo vizuri.
Mimi nilikwenda Mlimani City siku ile, kuna ndugu yangu alikuwa mmoja wa
watoa tuzo.
“Alipoona
kila anayepanda anadhalilishwa (ingawa kwa Mpoki ni utani) akaingiwa
hofu. Ilifika mahali akatamani kuahirisha kwenda kutoa tuzo, tukampa
moyo lakini alipopanda mambo yakawa yaleyale, akadhalilishwa waziwazi.
“Mpoki
anatakiwa kubadilika. Nampa ushauri wa bure, ajifunze kupitia kwa
wengine. Lakini hata hivyo mimi popote ambapo yeye atakuwa
mshereheshaji, sitakanyaga hata kwa dawa.”
Dulla wa
Sinza Kwaremmy alisema: “Sikufurahishwa na kitendo cha kumwambia Dj Bon
Love na wadogo zake kwamba ni wabahili wa fedha na kumshangaa Vanessa
Mdee kwa kuzungumza Kiingereza wakati yeye ni Mpare azungumze Kiswahili,
halafu akamkejeli eti awe anafanya mazoezi ya kuvaa viatu virefu baada
ya kunusurika kuanguka jukwaani. Ule si utani ni udhalilishaji.”
Mdau
mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema: “Sikufurahishwa
kabisa alivyomwambia Isha Mashauzi, eti ni mwanamke wa Kikurya, si wa
kuoa.
Lakini
mbaya zaidi akamwambia make up zilimfanya aonekane msichana mrembo,
lakini akiamka asubuhi atapewa shikamoo kwa mwonekano mpya
atakaokuwanao. Ile ilikuwa too much. Kifupi Mpoki ni mpuuzi sana.”
HUYU AWAKUMBUKA TAJI, MILLARD NA PENNY
January Kingamkono wa Msasani Dar, yeye alikwenda mbali zaidi na kuwakumbuka washereheshaji wa siku zote katika hafla hiyo, Taji Liundi, Millard Ayo, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na wengineo.

Hapa
anafafanua: “Kili walichemsha kwa kweli. Kumkaribisha Mpoki lilikuwa
wazo zuri lakini mizaha yake ilikuwa ya kijinga sana. Alikuwa akiwatusi
na kuwakejeli watu na si kuchekesha. Nawashauri Kili wafikirie
kuwarudisha akina Taji na wengine waliokuwa wakifanya vizuri kwa pamoja
kama kweli wanataka hafla yao iwe na msisimko.
“Wakumbuke
Tuzo za Kili siyo free event (onesho la bure), watu wanatoa pesa zao.
Sasa lazima wazingatie kuwa kinachotolewa kwa watazamaji kinalingana na
hela iliyolipwa. Kifupi Mpoki aliboa,” alisema Kingamkono.
HUYU ATAKA AOMBE RADHI
Mdau mwingine, Juma Alii wa Manzese ya Tip Top jijini Dar alisema: “Mpoki anatakiwa kujifunza. Kila kona sasa hivi gumzo ni yeye. Nasikia wale mastaa waliokejeliwa wanataka kumfungulia kesi, ni vyema ajifunze kusoma alama za nyakati. Ajue alikosea na aombe radhi.

“Lakini pia
ni vizuri kama atajifunza kutoka kwa washereheshaji wengine, namna
wanavyofanya kazi kwenye matukio rasmi kama hayo.”
TAJI ASHAURI
Mkongwe katika tasnia ya utangazaji Bongo, Taji Liundi aliona kasoro za Mpoki. Hata hivyo, kwa kutumia busara alitupia katika ukurasa wake ndani ya Mtandao wa Kijamii wa Facebook akizungumzia hafla hiyo ambapo aliandika: “Nadhani ingekuwa vema kutambulisha wasoma tuzo vizuri.

Kuna mtu
mmoja “Mhaya Mweupe” angestahili kuwasilisha kwa umakini zaidi!! Pia
tunasikia mazungumzo ya watangazaji na watu nyuma ya jukwaa kupitia mic
zisizozimwa. Onesho lina msisimko lakini nadhani “production” imekuwa na
changamoto!
Maneno hayo
yalitupiwa na Taji, Mei 4, mwaka huu muda mfupi tu wadau wakaibuka na
kulipuka. Wa kwanza alikuwa ni Dinne Shose ambaye aliandika:
“Yaani Taji
nimeliwaza hilo nikawa nawaambia wadogo zangu...imekuwaje? Wapi
Taji?...ma MC hawana mvuto...utani upo lakini hauchangamshi matokeo yake
utani umezidi hadi unaboa watu...wish Taji, Millard, Jokate na Penniel
mngekuwa ma MC.”
Mara moja,
Taji akajibu: “Dinne ahsante kwa maoni. Sisi wazoefu tutapata majukwaa
mengine. Nadhani Shadee kajitahidi sana lakini shoo ilikuwa ndefu, focus
inaweza kupotea. Mpoki katumia mtindo wa Kevin Hart akiwa ana-MC BET.”
TAJI AMTOLEA UVIVU
Baada ya mjadala kuwa mkali huku wachangiaji wengi wakipeleka lawama zao moja kwa moja kwa Mpoki, Taji aliamua kumtolea uvivu kwa kuandika hisia zake kwa ukweli kuhusu ubovu wa aliouita utani lakini kumbe ni udhalilishaji.

Sehemu
ya maandishi ya Taji yanasomeka: “Hakuna shaka kwamba Mpoki ni
mchekeshaji mzuri. Hapo juu nimeelezea mtindo wake wa kukejeli
alipoutoa. Ni kwa mchekeshaji mwenzake Kevin Hart. Je, alipitiliza?
Nadhani NDIYO. Kwa Bon Luv na Ray Kigosi. Sikumwelewa Mpoki. Nadhani
Martin Kadinda naye hakupendezwa.
“Hapo sasa
kuna tofauti ya KUCHEKESHA na KUBEZA, pia ya kuwa MC! Kasoro nyingine
niliyoiona ni kurusha watu, Fina, Ruge... Sijui kama ilikuwa kwenye
script. Mchango wa Fina unaeleweka kupitia OnePlus (kejeli za Mngoni
kuzaa na Mzungu hazikuwa na ladha).
“Naamini
Mpoki atapokea maoni chanya ili aweze kuji-balance akifungua mdomo.
Ajipange. Kuna kitu kinaitwa MANENO MATUPU, kama vile kujitangaza kuwa
ni MC wa harusi angali anafanya KTMA mara ya pili na kuaminika, masuala
ya kulipwa ontime mbele ya Kavishe???? Matani ya “kiutu uzima” kwenye
Live TV, watoto wanaangalia!!
“Anyway,
yote haya hayatakosa kukosolewa kwa tamasha kubwa kama lile. Nadhani
hakuna mchangiaji anayechukia KTMA. Kuomba ushauri wasiache.
Ikiwa watu
wanalewa ukumbini, unategemea nini kama nusu ukumbi ukiamka kumtuza,
kumtukana Diamond au kuwafuata wasanii backstage? Dah!! Kungekuwa na
bucket la maji kwa kila mchemshaji! Ni kusema lile tangazo nalo tata! Si
Sprite vile? Naona kama watu watamwagiana pombe??!”
MDAU MWINGINE
Edwine Ndaki alisema: “ Taji Liundi upo sahihi, nimependa ulifanya uchambuzi na ushauri. Kwa sisi tulio nje ya nchi tunapongeza kwa wazo la kurusha event live online. Mpoki next time au popote inabidi aangalie utani gani na wapi.”

JIMMY CHOCOLATE MKATTE
“Iko haja ya ma - MC kufanyiwa rotation, rafiki yangu Mpoki alibweteka akamnyima Co - MC nafasi. That was illegal.”
“Iko haja ya ma - MC kufanyiwa rotation, rafiki yangu Mpoki alibweteka akamnyima Co - MC nafasi. That was illegal.”
BINTI SHANGWE
“Kasoro kibao, MC wameboa, hakuna mpangilio, huyu hajamaliza kuongea, huyu kashadakia, hasa Mwarabu wa Dubai, mtu anayetaja jina la mshindi na MC inabidi wapokezane mic...”
“Kasoro kibao, MC wameboa, hakuna mpangilio, huyu hajamaliza kuongea, huyu kashadakia, hasa Mwarabu wa Dubai, mtu anayetaja jina la mshindi na MC inabidi wapokezane mic...”
KILI: HATUKUJUA KAMA ANGEHARIBU
Mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya tuzo hizo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa maelezo kuwa si msemaji, alizungumzia kuhusu udhalilishaji uliofanywa na Mpoki, akasema hawakujua kama angefanya vile.

“Tulimwamini
maana tulishawahi kufanya naye kazi. Kilichotokea pale kilitushangaza
sana lakini isingekuwa rahisi kumrekebisha wakati akiwa tayari yuko
jukwaani. Pengine utekelezaji wa hilo ungesababisha tatizo jingine kubwa
zaidi. Niseme tu, tumejifunza.”
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Mpoki, wewe ni staa na una heshima kubwa kwenye jamii. Kila binadamu amepewa akili; uwezo wa kufikiri upo kwa kila mmoja tatizo ni pale kwenye uamuzi wa kutumia. Ni vyema sasa ukabadilisha staili ya maisha na uanze kutumia akili yako ipasavyo.

Vichekesho
siyo kuwadhalilisha watu, lakini kubwa zaidi kumbuka ulipotoka, acha
kuwakejeli hadi waliokusaidia – hata hivyo si uungwana kuwadhalilisha
watu.
Badilika ili uondoke kwenye ujinga kwa kuchekesha vitu vyenye mantiki ili uwe mwerevu. Inawezekana ukiamua! – MHARIRI.
Badilika ili uondoke kwenye ujinga kwa kuchekesha vitu vyenye mantiki ili uwe mwerevu. Inawezekana ukiamua! – MHARIRI.
source; GPL