MTANGAZAJI wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’
amewashtua mashabiki wake baada ya kutupia picha kwenye mtandao wa
Instagram ikionesha sehemu kubwa ya tumbo lake likiwa wazi.
Mtangazaji wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya picha hiyo kuzagaa
mitandaoni, Penny alisema ameitupia picha hiyo kuonesha alivyokuwa
mazoezini akiwa amechoka na kujilaza hivyo asielewekevibaya.
Peniel Mungilwa ‘Penny’ akiwa kwenye pozi.
“Nimeanza mazoezi ya nguvu sana na tayari nimeshapungua karibu kilo
10, nimefanya hivyo kwa nia ya kuuweka sawa mwili wangu, nisieleweke
vibaya,” alisema Penny.