Aisha Iddi mkazi wa Ilala Dar es salaam amefanya exclusive interview kupitia sammisago.com kuhusu kipigo alichopokea kutoka kwa Msanii Chid Benz na sababu ya kupigwa hivyo.
Aisha
anasema” Chid nafahamiana naye kama mshkaji tu na nilimsalimia akiwa na
mwanamke, nadhani hakufurahishwa na kitendo hicho , akachukia na kuanza
kunipiga, kwanza alianza kurusha meza kwenye bar tuliyokuweko ya Ngudu
Bar iliyopo ilala”
Aisha
anaendelea kusema” Chid amemchana vibaya mdomoni mpaka kusababisha
kushonwa nyuzi 13 mdomoni. pia amenivuta rasta kichwani mpaka ikatoka,
Niko kwenye hali mbaya sana nikiachwa mwenyewe nazimia ”
Kwa sasa kesi ipo mahakamani baada ya Chid kukamatwa kupitia Rb – ILA| RB | 1569| 2014 Kituo cha polisi cha Pangani Ilala.