Listi maarufu sana ya wasanii wa Hiphop wenye pesa nyingi hatimaye
imetoka tena kwa mwaka 2014 na sura zikiwa zilezile lakini kuna
waliopanda sana na wengine wameshuka kwenye nafasi zao.
P Diddy anaweza kuwa msanii wa kwanza wa Hiphop kuwa billionea kwenye
miaka michache ijayo kutokana na kasi yake ya kuingiza pesa nyingi na
uwekezaji wenye faida kubwa nje ya muziki.
Namba moja kwenye hii listi imekamatwa na P.Diddy ambaye kutokana na
mkataba wake mpya na kampuni ya Diageo ambapo bado anahusika na
usimamizi wa brand ya Ciroc lakini pia DeLeon Tequila imeongezeka na
kuongeza mapato kwake.
Revolt TV anayomiliki P Diddy ambayo imeanza kwa kasi kubwa ndiyo
biashara inayosemekana kuwa inaweza kumfanya Diddy kubwa bilionea wa
kwanza kwenye HipHop.
Mwaka jana alikuwa na utajari wa dola millioni 580 lakini ndani ya
mwaka mmoja ameingiza dola millioni 120 na kufanya utajiri wake kuwa na
jumla ya dola za kimarekani millioni 700.Namba mbili ni ya producer na msanii Dr Dre ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani millioni 550.Namba tatu inaenda kwa Jay Z utajiri wake ni dola za kimarekani millioni 520.Namba nne ni ya boss wa YMCMB ‘Birdman’ utajiri wake ni dola za kimarakani millioni 160.Namba tano inamilikiwa na 50 Cent ambaye utajiri wake ni dola za kimarekani millioni 140.