Ni mmoja kati ya wasanii kutoka Afrika Mashariki Judith Wambura a.k.a
Lady Jay Dee amepata ‘shavu’ la kuimba katika wimbo wa Kombe la Dunia
mwaka 2014(FIFA World Cup Anthem 2014) akiwa yupo na wasanii wengine
kama David Correy kutoka Brazil na Rapper Octoppizo kutoka Nchini Kenya.
Katika hiyo ngoma Lady Jay Dee na David Correy wameimba kwa kutumia
lugha ya kiingereza huku Octoppizo akiwa amerap kwa lugha ya kiswahili.
Wimbo huo ambao umetambulishwa na Kampuni ya Coca Cola wakiwa wanazindua
promosheni yao ya Kombe la Dunia itakayowezesha wateja wao kujishindia
zawadi mbalimbali.
Tuliweza kushiriki Coke Studio mwaka jana na nyimbo mbalimbali
tulikuwa tunafanya zikiwemo nyimbo zetu wenyewe na zingine za copy, na
moja kitu tulichofanya ni kurekodi wimbo kwa ajili ya Kombe la Dunia,
kwa hivyo tulikuwa wasanii wengi mbalimbali wengine kutoka Nigeria,South
Afrika, Tanzania, Uganda na Kenya, kwa hivyo baada ya hapo tulikuwa
tunasubiri huu wimbo uweze kutoka, na hatukufanyiwa audition ni wasanii
walewale tuliochaguliwa kutoka nchi nane za Afrika, kwenda kule ndiyo
tukarekodi baada ya hapo kikatoka kilichotoka, na ni wimbo mzuri ambao
umechangamka na unaongelea tu kuhamasisha watu kuhusiana na soka na vitu
kama hivyo”. Lady Jay Dee