Siku mbili zilizopita stori mbalimbali kwenye mitandao zilihusu
msanii wa longtime kwenye bongofleva aitwae Dudubaya kudaiwa kumkata
sikia Mama yake mkubwa kwa kinachosemekana kuwa tuhuma za kichawi lakini
siku moja baadae Dudubaya alikanusha kupitia U Heard ya XXL Clouds FM
kwamba hajamkata bibi yake sikio, yeye sio mtu wa kufanya hicho kitendo.
Sasa leo Mama mkubwa huyu wa Dudubaya amezungumza na Waandishi wa
habari na kuthibitisha kweli kukatwa sikio na Dudubaya ambapo shahidi
mwingine aliezungumza ni mjukuu wake.
Maelezo waliyoyatoa ambayo ndio yamenifikia sasa hivi yatawekwa hapa on millardayo.com baadae lakini pia yatasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo usiku.