Unaweza
kuichukulia kivyovyote lakini maandishi ya member wa Tamaduni Music,
Nash MC yameeleza wazi kuwa anamzimia mrembo na mwimbaji wa kundi la
Shosteez, Meninah la Diva.
Comment ya Nash MC aliyoiweka kwenye
post ya Jabir Saleh a.k.a Kuvichaka aliyokuwa ameweka kwenye ukurasa wa
Facebook akiwa na Dayna Nyange ambaye atakuwa mkali wa The Jump Off
kuanzia wiki ijayo, ilikuwa na ujumbe wa wazi kwa mtangazaji huyo.
“Siku ukimhoji menina nistue maana mamzimia kweli.” Aliandika Nash MC.
Hata hivyo, ujumbe huo haukuishia kwa
Kuvichaka na akaupeleka kwa watu wengine ambao wanaweza kukutana na
Meninah au wale ambao walidhani ametereza tu kuandika kwa uwazi.
“Hilo lipo wazi na mkimuona mwambieni.” Alisisitiza Nash MC.
Rapper huyo wa Naandika alijitoa kwenye
lawama binafsi na kuchombeza kiutani kuwa kilichomsukuma na upendo.
“Sio mm ni sababu ya mapendooooooo!”