Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia
fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya
kuifunga Marekani goli 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali
uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro Brazil.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa goli
4-0,goli pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali
ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho za mchezo huo.
Kwa matokeo haya Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi,Mechi hiyo
inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo
baada ya kuifunga Pakistan goli 4-3 katika nusu fainali ya pili.
Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya
Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi akiwa
Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo,Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.