Kwa sasa bongo ukizungumzia watayarishaji wa muziki wa kizazi kipya wanaofanya vizuri huwezi kuacha kumzungumzia Messen kutoka D Fatality Music,ambaye anafanya kazi zake hapo,Kipindi cha nyuma Messen alikuwa anafanyia kazi zake sebuleni kwao, ambapo alikuwa anapata shida wakati akiwa anataka hasa kuingiza vocal, hapo ni lazima madirisha yafungwe na kila mtu akae kimya.
Lakini siku kadri zilivyozidi kwenda na kazi zinafanyika za maana kwa mujibu wa Messen ikabidi afanye mpango wa kutengeneza ofisi yake kwao hapo hapo, ambapo hadi sasa ameshagharamikia takribani milioni 30 katika ujenzi na vifaa vya studio lakini bado haijakamilika kama anavyotaka iwe.