Tuesday, November 12, 2013

P-FUNK APATA AJALI YA KUSHANGAZA CHOONI

0
LEGEND wa kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.
Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.
KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.
‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.
“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?
Chooni alipodondoka P-Funky na kupata majeruhi kichwani.
P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.
Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.
Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment