Mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana.
MTANGAZAJI na mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana, atazikwa mjini Tabora.Safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Tabora inategemewa kuanza kati ya saa 10 na saa 11 leo alasiri.Mwili wa Nyawana ambao uko chumba cha kuhifadhia Hospitali ya Mwananyamala, unatarajiwa kuchukuliwa muda wowote kuanzia saa 7 kwaajili ya kwenda kuoshwa msikitini kabla haujapelekwa nyumbani kwao Magomeni Makanya (jirani na Bibi Nyau) ambako ndipo msiba ulipo. Nyawana ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Tabora kunako mwaka 1986, alizaliwa jijini Dar es Saaam miaka 36 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Msanii huyo aliyepitia vikundi vya Kings Modern Taarab na Tanzania Moto Modern Taarab alitamba zaidi akiwa kama msanii wa kujitegemea (solo artist) huku wimbo uliomtambulisha ukijulikana kama “Nipo Kamili Nimejipanga” uliotoka mwaka 2011 utunzi wake Thabit Abdul Wimbo wake wa pili ulijulikana kama “Umesharoga Wangapi” wakati wimbo wake wa mwisho aliouachia hivi karibuni ulikwenda kwa jina la “Shetani Kataja jina”.Nyawana anategemewa kuzikwa kesho Jumatano mjini Tabora, sehemu ambayo inaaminika alijizolea umaarufu mkubwa zaidi kwa kazi yake ya utangazaji na baadae uimbaji.Kimahusiano, Nyawana alifunga ndoa na mdau mkubwa wa taarab Kaisi Mussa Kaisimmiezi kadhaa iliyopita.
Akiongea jana mchana Hospital ya Mwananyamala wakati wa kwenda kuhifadhi mwili wa marehmu, mumewe Kasi Mussa alisema siku zote mkewe alikuwa akimweleza kuwa iwapo atatangulia kufariki basi mwili wake ukazikwe Tabora.
Mara nyingi sana alikuwa akiirudia hii kauli, wakati mwingine hata tukiwa katika hali ya furaha na kutaniana lakini bado aliingiza hiyo kauli,” alisema Kaisi Mussa Kai
Chanzo Saluti 5