Pamoja na mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Danie Levy na kocha Andre Villas-Boas kusema mara kwa mara kwamba Gareth Bale hatouzwa kwenda popote msimu huu - lakini leo hii gazeti la kihispania la Marca kimeripoti kwenye ukurasa wake wa mbele kwamba Gareth Bale ameshakubaliana kimsingi na Real Madrid kuhamia kwenye klabu hiyo.
Marca wameripoti kwamba Real wamempa ofa ya mkataba wa miaka sita Bale na mshahara wa £8.5million kwa mwaka.
Marca pia imesema kwamba Bale ameiambia rasmi klabu yake kwamba anataka kwenda Santiago Bernabeu.
Gazeti hili lenye maskani yake jijini Madrid lina uhusiano wa karibu na klabu ya Real Madrid, na siku zote usajili mkubwa wa klabu hiyo umekuwa ukiripotiwa kwanza na gazeti hilo.
Inaaminika mara tu Marca wanapoandika habari ya Madrid kufanikisha usajili wa mchezaji yoyote na kumuweka kwenye ukurasa mbele wa gazeti hilo basi amini kifuatacho ni kukamilika kwa usajili huo. Ni mara chache sana gazeti hilo huandikahabari sio za kweli.
Usajili wa wachezaji kama Luka Modric, Cristiano Ronaldo na Kaka - wote ulianza kuandikwa kwanza kwenye gazeti la MARCA na mwishowe kweli wachezaji hao walisajiliwa na klabu hiyo.
Waliandika kuhusu kusajliwa kwa Modric na kweli ilitokea
Je Spurs wataweza kuvunja rekodi ya MARCA kuripoti usajili wa wachezaji na kweli usajili huo ukafanikiwa?Muda utaongea........http://www.shaffihdauda.com/ |