Linux Mint ni moja ya programu endeshi kongwe na pendwa sana na wataalam wa kompyuta. Pia, hupendwa na watu wanaoanza kujifunza teknolojia.
Hii inatokana na urahisi wake kuiweka katika kompyuta na ufanisi wake kuwa na kasi sana. Vilevile, kama programu endeshi zingine za familia/jamii ya Linux, inaweza kufanya kazi kwa ufanisi mzuri hata kwa kompyuta yenye sifa/uwezo wa kawaida.
Kama tunavyojua programu endeshaji (OS) nyingi za familia/jamii ya Linux huwa zinapatikana bure/bila malipo. Programu endeshi hizi zinatumia Kernel ya LINUX ambayo hujulikana kama moyo wa hizi programu endeshi zote za bure kama vile Ubuntu, Fedora, Manjaro, Kali Linux na kadhalika. Linux Mint 19.2 inayotambulika kwa jina la “TINA” imetoka mnamo tarehe 02.08.2019 ikiwa na vitu vipya pamoja na marekebisho.
Linux Mint ni moja ya programu endeshi ambayo inatumika vyuoni hata hapa Tanzania kuna vyuo vingi vinavyotoa elimu ya teknolojia vinavyotumia programu endeshi husika kufundushia. Mfano wa chuo kinachotumia programu endeshi hii ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Unaweza pitia hapa kwenye tovuti yao kuifahamu zaidi na kudownload programu hii endeshi kwa ajili ya kuweka kwenye kompyuta yako – inaweza wekwa kwenye kompyuta mpakato au za kawaida.
Toleo kwa ajili ya kompyuta za mezani | 32 bit | 64 bit |
CINNAMON | pakua | pakua |
MATE | pakua | pakua |
XFCE | pakuua | pakua |
Kumbuka faida za kutumia programu endeshaji za Linux ni pamoja na:
- Kuepuka mashambulizi ya virusi; virusi vingi vya kompyuta vinatengenezwa kwa ajili ya Windows, na pia usalama mwingine kwenye programu endeshaji za Linux ni pamoja na kutakiwa kuingiza nywila (neno siri) ya kompyuta kabla ya kupakua programu yoyote kwenye kompyuta.
- Pata programu za bure: Programu nyingi kwa ajili ya programu endeshaji hizi zinapatikana BURE (bila malipo). Hii inajumuhisha programu kama vile za kazi za uandishi, programu za kufanyia kazi picha au video.
- Pia uwezo wa kutumia programu za Windows unawezekana kupitia programu spesheli inayotakiwa kupakuliwa kwenye programu endeshaji ya Linux. Inafahamika kwa jina la Wine, programu hii itakuwezesha kupakua na kutumia programu za Windows kama vile Word, PowerPoint na pia ata kucheza baadhi ya magemu ya Windows.