TikTok ni mtandao wa kijamii ambao umejipatia umaarufu mkubwa sana kwa umahiri wake. ukiachana na umaarufu ni kwamba iko wazi kuwa mtandao huo unapendwa na watu wengi sana. TikTok ni mtandao wa kijamii wa kutengeneza video mbali mbali na kuzi’share na marafiki..
Inapatikana katika Android na iOS, App hiyo maarufu imetengenezwa na kampuni ya ByteDance. kampuni mama hiyo ina App nyingi sana chini yake.. kwa sasa imeweka wazi kwa dunia kwamba haipo katika kutegemea kitu kimoja tuu (Apps).
Ni sawa wana App nyingi tuu lakini ile maarufu kuliko zote imebaki kuwa ni TikTok ambayo mpaka sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani kote. Ukiachana na hayo yote bado mtandao huu umeshangaza wengi kwani unakua kwa kasi sana kuliko hata mitandao mingine mikubwa ambayo tunakuwa tumeizoea.
Mwezi februari mwaka huu App hiyo ya TikTok ilipiga hatua na kuwa imeshushwa zaidi ya mara bilioni moja. TikTok ni moja ya App ambayo inashikilia rekodi ya kujikuza yenyewe mpaka kufikia kuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 75..
Kampuni mama ambayo ni ByteDance imweka wazi kuwa kuna vitu vingine vingi tuu vya kufanya ukiachana kuitegemea App hiyo na nyingine ambazo inazo.. ni wazi makampuni mengi yanajiingiza katika soko la simu.. kitu hichi kilishafanywa na microsoft, vile vile kampuni kama google na Amazon wote wameenda na kuanzisha kampuni zingine za kuzalisha simu janja au vifaa vya simu.
Chombo cha habari kutoka china kimeweka wazi kuwa mpaka sasa imeshapita miezi 7 tangia kazi ya kutengeneza simu janja hizo ianze rasmi… bila shaka hili ni jambo zuri sana kwao ByteDance.