Kumbe Diamond sio wa mchezo. Hivi ndio vitu ambavyo amejitolea kusaidi jamii mpaka sasa.Hilo limekuja baada ya shabiki mmoja kuandika ujumbe ambao ulionekana kumgusa muimbaji huyo. “……100m Kwenye shingo…huku watu wana ishu nashida atleast wasaidie watu kwenye maeneo mabaya,” alicomment shabiki huyo kwenye picha hiyo hapo chini.Naye Diamond alimjibu kwa kuandika, ““…..nimejenga nyumba 5 mwaka jana Iringa, misikiti miwili mmoja Morogoro pia nyingine Mtwara na madrasa Tegeta na nyumba ya Imamu mbali na sadaka mbali mbali sasa unataka nitoe hela zote sadaka nami nisifurahishe ebu niombe radhi kwa hilo.”